16 Machi 2012 - 20:30

mawaziri wa mambo ya nje ya Tunis, Libya na Misri katika kikao cha pamoja baina ya nchi hizo nchini Tunis, wamesisitiza utatuzi wa machafuko ya Syria chini ya uangalizi wa umoja wa waarabu, na kutoafiki kwao nchi za nje kuingilia masuala ya Syria.

Rafiki Abdu salam waziri wa mambo ya nje nchini Tunis siku ya ijumaa baada ya mkutano uliohudhuriwa na mawaziri wa Misri na Libya ametoa wito wa kutatuliwa machafuko ya Syria chini ya umoja wa kiarabu na kupinga nchi za nje kuingilia mambo ya Syria. waziri huyo amesema: unyama na umwagaji damu nchini Syria unapaswa kusitishwa haraka iwezekanvyo, pamoja yakuwa haitawezekana kurudi katika hali yake ya zamani kwa sababu wananchi wa Syria wanamahitaji yao kikanuni kwa Serikali na serikali inapaswa kutekeleza matakwa hayo na kuyazingatia. mawaziri wa mambo ya nje ya Misri Tunis na Libya wametoa ujumbi kwasauti moja kwa kupigavitendo vya kigaidi na mauaji kwa watu wasio na hatia.